Breaking News

USAJILI WA GRIEZMANN: MOURINHO ABADILI GIA ANGANI

Baada ya tetesi kuvuma duniani kote kuwa Klabu ya Manchester United ipo mbioni kunasa saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann hatimae mashetani wekundu wamtolea nje mshambuliaji huyo.



Taarifa kutoka mtandao wa Daily Mail zinaeleza kuwa kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho ameamua kumpotezea Griezmann huku akitajwa kumfukuzia Romelu Lukaku wa Everton pamoja na Andrea Belotti na Alvaro Morata.

Mpango wa kumnasa Griezmann unaonekana kufeli baada ya Atletico Madrid kupoteza rufaa yao ya kupinga kuzuia kusajili kufuatia adhabu ya kukiuka masharti ya uhamisho wa chipukizi walio chini ya umri wa maka 18.