Breaking News

SASHA AKERWA SAUTI YAKE KUFANANISHWA NA WEMA SEPETU


MWA­NA­MITINDO, Sasha Kas­sim ameibuka na kusema kuwa hapendi sauti yake kufananishwa na ya Wema Sepetu kwani inaanza kumletea matatizo am­bayo hakuyatarajia kwa maana ya usumbufu.



Sasha alion­gea hayo baada ya kuandam­wa na watu aki­daiwa kuhusika na utengenezaji wa sauti iliyokuwa ikisambaa mtandaoni kitendo ambacho alikana kukifanya na kudai kuwa hana mazoea wala maisha hayo ya kujianika kwa kutafuta kiki.


Dah mimi sija­husika na sauti yoy­ote na wala sidhani kama sauti yangu inafanana kiasi hicho na Wema kwamba naweza ku­muigiza mimi si wa hivyo jamani ki­tendo cha kuhusishwa na sauti hiyo kimeni­kera na naomba watu waache mara moja,” alisema Sa­sha.