RIPOTI YA UCHUNGUZI MCHANGA WA MADINI YAMUONDOA WAZIRI SOSPETER MUHONGO... RAIS MAGUFULI AMTAKA AACHE KAZI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA
Rais
John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo kuachia madaraka kwa kushindwa kusimamia suala la mchanga wa
dhahabu unaosafirishwa kwenye makontena.
Amemtaka waziri huyo kujitathimini na bila kuchukua muda mrefu aachie madaraka kutokana na suala hilo.
Rais Magufuli amesema hayo baada ya kamati iliyokuwa ikichunguza suala la mchanga kwenye makontena kukabidhi ripoti yao.
Kamati
hiyo ya wataalamu wa jiolojia na uchambuzi wa kisayansi iliyoundwa
Machi 29 mwaka huu, ilichunguza aina ya madini yaliyopo, kiasi na
viwango vya ubora.
Akikabidhi
ripoti hiyo, Profesa Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa
madini ya kiasi cha kati ya Sh829.4 bilioni mpaka 1.439 Trillion kwa
makontena yote 277.
"Licha
ya uchunguzi uliofanywa kupitia makontena haya, tumegundua uwepo wa
aina nyingi zaidi za madini ambayo hayakuwa yakijulikana na haya
yamekutwa na thamani ya kati Sh129.5 bilioni mpaka261 bilioni," amesema Profesa Mruma.