Breaking News

RAIS DONALD TRUMP ZIARANI NCHINI SAUDI ARABIA


Rais wa Marekani Dolnad Trump amefanya ziara yake katika nchi ya Saudia , huku ziara hiyo ikitarajiwa kuwa ya siku nane tu, itakayo shirikisha nchi za Israel,Palestina,Ubelgiji,Vatican na Sicily.
Rais Trump yupo katika ziara hiyo na mkewe Melania na wamepokelea leo Alfariji na Mfalme wa Saudia. Mikataba mbali mbali ya mabilioni inatarajiwa kutiwa saini kati ya nchi hizo mbili,huku ziara hiyo ikiwa ni ya kwanza kwa bwana Trump kufanya Saudia, tangu aingie madarakani.
Kwa upande wa Rais Omar el-Bashir wa Sudan, yeye amekataa kuhudhuria mwaliko wa mkutano wa mataifa ya kiislamu ambao Trump atakuwa mgeni rasmi.
Bw.Bashir ametoa sababu binafsi za kutokuhudhuria mkutano huo. Hata hivyo Rais huyo wa Sudan anasakwa kwa kuchochea uhalifu wa kivita katika eneo la Darfur, na Marekani haikufurahishwa na mualiko wake katika mkutano huo.