PICHA: KIJANA AMUUA MPENZI WAKE KISHA KUENDELEA KUFANYA MAPENZI NA MAITI HIYO
Mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina la Timothy Johnson mwenye umri wa
miaka 25, anashikiliwa na Jeshi la Polisi la Florida nchini Marekani kwa
kosa la kumuua mpenzi wake Judith Therianos aliyekuwa na umri wa miaka
52, na kisha kuendelea kufanya naye mapenzi kwa muda.
Taarifa zilizotolewa na Mkuu wa kitengo cha polisi cha Florida, Chris
Nocco zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea mwezi uliopita wakati wawili
hao walipokuwa wanafanya mapenzi.
Nocco aliwaeleza waandishi wa habari kuwa uchunguzi wa polisi umebaini
kuwa wakati wanaendelea kufanya mapenzi, mwanamke huyo alimtaka
mtuhumiwa kutoendelea na ndipo alipomuua na kisha kuendelea na zoezi
hilo kwa muda.
Kwa mujibu wa Polisi, Judith hakuonekana tangu Machi 14 mwaka huu kabla
ya kubainika kuwa alikuwa ameuawa baada ya mwili wake kupatikana Aprili
7.