Breaking News

MKUU WA WILAYA YA ILALA AFUNGUKA MENGI KUHUSU MAISHA YAKE....INGIA NDANI UJIONEE




Hivi karibuni gazeti moja la udaku linalosifika kwa kuchimbua undani wa maisha ya watu maarufu, lilipiga hodi oļ¬sini kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Soļ¬a Mjema na kufanya naye mazungumzo, ambapo pamoja na mambo mengine, alifunguka mengi yaliyojiļ¬cha kuhusu maisha yake ya kimapenzi na safari yake nzima kimaisha hadi leo kukalia nafasi aliyonayo, msikie hapa chini akianza na historia yake:

“Naitwa Soļ¬a Mjema, nimezaliwa zaidi ya miaka 46 iliyopita huko mkoani Kilimanjaro, Gonja –Maole upareni, ingawa nimekulia hapa jijini Dar baada ya baba yangu kuja kusoma udaktari, hivyo nimesoma shule za msingi na sekondari hapahapa,” anaanza kusimulia mheshimiwa huyo.
“Nilianza masomo ya darasa la kwanza nikiwa mdogo sana, miaka minne na nusu, darasa la kwanza nimesoma Shule ya Msingi Bunge, lakini baadaye nilihamia Olympio ambako sikudumu sana kwa sababu serikali iliamua kubadilisha baadhi ya shule kuwa za Kiingereza, hivyo nilihamia Shule ya Msingi Muhimbili na kuhitimu elimu ya msingi,” anasema na kuendelea;
“Kidato cha kwanza hadi cha nne nimesoma Shule ya Sekondari Kisutu na Kidato cha Tano na Sita nilisoma Jangwani.” Hapohapo, mkuu huyo wa wilaya anaongeza: “Nilipohitimu nilijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), nilikwenda Ruvu mwaka mmoja, lakini pia baada ya kuhitimu nilianza kusoma kozi mbalimbali fupifupi na baadaye kupata udhamini wa masomo (scholarship) nchini Uingereza, kwenye Chuo Kikuu cha Sunderland nikichukua kozi ya CBIS (Computer Basic Information System), nikijifunza namna ya kutengeneza mifumo (programs ) mbalimbali kisha nikarejea nchini kuanza kufanya kazi na Carts Computers, kabla sijaanza kufanya kazi na BP (British Petroleum) upande wa marketing,” anasema.
KWENYE SIASA
“Mwaka 2005 niliamua kujiingiza kwenye siasa, niliona sasa nafaa kuwatumikia wananchi katika nafasi hiyo, nilikwenda mkoani kwetu kupigania nafasi ya special seats (viti maalum), tulikuwa wanawake 57 na niliambulia nafasi ya tano, hivyo nikashukuru Mungu na kurejea tena kazini kwangu kwa kuwa niliondoka katika mazigira raļ¬ ki,” anasimulia kwa utulivu na uchangamfu.
“Lakini mwaka 2006, mwezi wa nane nakumbuka ilikuwa saa 12 nilipigiwa simu na mbunge mmoja akinieleza kama nimesikia kwenye taarifa ya habari nikamjibu hapana, akasema nimeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, nikasubiri habari ya saa mbili, kweli mheshimiwa rais alikuwa ameniteua nikamwakilishe kwenye Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga,” anasema na kuendelea;
“Nikaenda kushika nafasi, lakini nilikuwa na miaka 25 tu, hivyo mimi ndiye nilikuwa mkuu wa wilaya mwenye umri mdogo kabisa kuliko wote, niliuliza majukumu ya mkuu wa wilaya ni yapi maana sikuwa najua kitu. Lakini nilifanikiwa na kukaa pale Lushoto kwa zaidi ya miaka sita na nusu, kulikuwepo na mabadiliko mengi pale katikati, lakini mimi niliendelea kubakizwa palepale Lushoto, ndipo mwaka 2012 nilihamishiwa Temeke ambako nilikaa miaka minne na sasa niko hapa Ilala,” anasema Soļ¬a.
MAISHA BINAFSI SASA
Gazeti la Ijumaa linamdodosa DC huyu kuhusu maisha yake binafsi, nje na ulingo wa siasa na utumishi wa umma ambapo anaainisha baadhi ya mambo mengi yaliyo nyuma ya pazia. Bi. Mjema anasema ameolewa na ana watoto wawili na mmoja wa kuasili, ambaye anamsaidia kwa mambo mbalimbali, huku akiweka wazi kuwa katika maisha yake anapenda sana muziki.
“Nikiwa nyumbani nafanya kazi kama mama na mke wa mtu, napika kama kawaida na unajua mama yangu naishi naye na sasa ni mtu mzima hivyo wakati mwingine lazima nimuandalie chakula, pia nagawa muda wangu wa kazi na familia, wanangu wanaelewa, muda wa nyumbani nakuwa nao, nikiwa kazini wanajua na wakati mwingine nafanya kazi hadi Jumamosi na Jumapili,” anasema na kuongeza;
“Nafurahia ndoa yangu, siyo kwamba haina migogoro, lakini sipendi kuzungumzia upande huo lakini nataka kusisitiza kwenye uadilifu na namna ya mtu kujitambua na kujipa nafasi ya kujua lipi ni lipi na nini kifanyike kwa wakati gani, uzuri wa mtu au kitu hudhihirika machoni mwa mtazamaji. Maisha yake ya kimapenzi Aidha, akimtazama mwandishi wetu kwa macho ya ‘unanichimba’,
Bi. Soļ¬ a aliweka wazi alivyokutana na mumewe, ambapo alisema walianzisha uhusiano wakiwa wanafanya kazi eneo moja, zaidi ya miaka 25 iliyopita na kwamba mumewe hakuwahi kumtamkia neno nakupenda.
“Bahati nzuri mume wangu naye alikuwa kijana mwenye maadili mazuri, hakuniambia neno nakupenda, hiyo lugha haikuwepo kwa kweli, tulianza na uraļ¬ ki, siku moja akaniomba anataka kunitembelea nyumbani, siku hiyo aliniuliza kama kuna chai nami nikamkubalia, hivyo alipoļ¬ ka nyumbani akamwambia mama yangu kuwa ananipenda na kwamba anataka kunioa.
“Mimi na mume wangu tulikuwa na uhusiano salama kabisa, hayo mengine yalifanyika baada ya kufunga ndoa, nina miaka 22 kwenye ndoa sasa na maisha yanaendelea.” Kwa muonekano wewe ni mwanamke mrembo sana, vipi usumbufu unaokutana nao kutoka kwa wanaume wakware?’ namuuliza huku nikimtazama kwa umakini zaidi.
“Mimi kama mwanamke, usumbufu lazima uwepo lakini ukiwa kiongozi, lazima utambue misingi ya maadili inayokuongoza na kujilinda vyema, kama kiongozi wa kitaifa, kujitambua ni jambo muhimu sana,” anasema kiongozi huyo.
NENO LAKE KWA WANANDOA
“Wanawake wengi hususan warembo, hawadumu kwenye ndoa au uhusiano kwa sababu ya kuringia uzuri wao, unadhani nini tatizo zaidi? “Uzuri kitu gani bwana? Kuna mtu anakula uzuri maishani? Warembo wanazaliwa kila siku, ukigeuka huku utasema huyu mzuri jamani, ukiangalia na kule unasema huyu ndiye kiboko zaidi, kama nilivyosema huko nyuma, mtu ni kujitambua hakuna aliyewahi kufaidika na uzuri kwa kukaa tu, muhimu ni kuchakarika na kuhakikisha ndoto na malengo kutimia, kuheshimu ndoa na uhusiano kwa ujumla, maana umri nao haumsubiri mtu,” anasema.
MAISHA YAKE YA KAZI YAKOJE?
“Kila siku ni kukimbiza ndoto. Bahati nzuri rais wetu ni mtu mwenye ndoto za kuleta mabadiliko, sijui niiweke vipi hii, lakini ni mtu anayeota ndoto na akiamka anapambana kuileta kwenye uhalisia, sijui kama naeleweka sana, lakini maisha ni kupigana na hakuna kulala kwa kweli.”
STAREHE ZAKE NI ZIPI?
“Sina starehe kubwa sana, sinywi pombe na sitafanya hivyo, zaidi sana napenda kujisomea vitabu mbalimbali ili kuongeza maarifa kuhusu maisha na uongozi kwa ujumla, hayo ndiyo maisha yangu ndani na nje ya siasa,” anasema mheshimiwa huyo anayeonekana kuwa ‘social’ sana