MBUNGE JOSEPH KASHEKU(MSUKUMA):WASUKUMA TUTAZILOGA NG'OMBE ZETU ILI MTAKAOKULA MVIMBE MATUMBO
Mbunge
wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amesema hawezi kumsifia hata
kidogo Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Maliasili na Utalii kwani yeye
na watu wake wa Wizara wanafanya mambo ya ajabu hasa kwa watu wa Kanda
ya Ziwa.
Musukuma
anasema watu wa Wizara ya Maliasili wamekuwa wakiuza ng'ombe za watu
jamii ya wasukuma na kuzipiga mnada kwa dili kwa lengo la kujinufaisha
wenyewe, hivyo mbunge huyo amesema wasukuma wameamua kuwa wataziroga
ng'ombe zote ili wanaokula ngo'mbe hizo Dar es Salaam wavimbe matumbo.
"Napata
shida sana kujiuliza labda sisi watu wa kanda ya ziwa labda tulikuja
kwa bahati mbaya Tanzania hii, mbona yanayofanyika Kanda ya Ziwa
hayafanyiki Kanda ya Kaskazini wakati nao wana mapori, Waziri ametoa
siku tatu tukamatiwe ng'ombe kwa kisingizio kwamba ni ng'ombe za
Wanyarwanda wakati huo huo watumishi wake wanaowaingiza Wanyarwanda
wanawaambia toeni ng'ombe, mnaenda kukamata ng'ombe za Wasukuma halafu
unazipiga mnada na mnada wenyewe unavyopigwa ni wa dili" alisisitiza Musukuma
Mbunge huyo aliendelea kuelezea namna watu wa Wizara ya Maliasili wanavyofanya minada hiyo huku wakiwaumiza wafugaji
"Yaani
ng'ombe 600 unaambiwa ulete milioni tatu halafu wanatoa watu wao wa
Ubungo sasa hapo nikupongeze kwa sababu gani? Tunajua mipango
inayoendelea kwenye wizara yako na niliwapigia kabisa watumishi wako,
wananiambia mliipenda wenyewe kwa kauli yake kama Mwenyekiti wa Chama
kesho yake akapiga ng'ombe za watu mnada yaani ng'ombe 500 zinauzwa
milioni tatu" alisema Musukuma
Joseph Msukuma aliendelea na msimamo wake
"Nataka
nikwambie sisi Wasukuma sasa tumeamua na ninazungumza uelewe tutaziroga
hizo ng'ombe mtavimba matumbo mnaozila huko Dar es Salaam,
haiwezekani kwanini wanunuzi watoke Dar es Salaam peke yake yaani leo
siku ya mnada watu wametoka na malori Pugu wamejuaje kama wanakuja
kushinda kwenye minada. Mnatukamatia ng'ombe hivi hii serikali imekosa
sehemu ya kukusanya hela mpaka mkanyang'anye ng'ombe za wafugaji
haiwezekani Mh. Maghembe"