MAALIM SEIF NA ASKOFU GWAJIMA KUKUTANA LEO SAA KUMI.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, leo saa 10 jioni atamtembelea Askofu Josephat Gwajima ofisini kwake Kanisani, Ubungo.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na
Mahusiano wa CUF, Mbarara Maharagande imeeleza kuwa Maalim Seif
anakwenda kumjulia hali Askofu Gwajima kumfariji na kuzungumza naye
masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.
Maalim Seif amekuwepo Dar es Salaam kikazi kwa siku kadhaa sasa ambapo pia amevitembelea vyombo mbalimbali vya habari.


