SIRRO:WANANCHI ACHENI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI...VIACHIENI VYOMBO HUSIKA.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro
amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi badala yake
waviachie vyombo husika ili viweze kufanya kazi yake.
Ameyasema
hayo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa wananchi kujichukulia sheria mikononi pindi wawakamatapo
watuhumiwa ni kinyume cha sheria hivyo wanatakiwa kuacha mara moja tabia
hiyo.
“Ni vyema wananchi wakaacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi ili vyombo usika vifanye kazi yake,”amesema Sirro.
Aidha,
amesema kuwa wananchi kuwauwa watuhumiwa ni kosa kisheria kwani watakao
bainika kufanya hivyo sheria kali dhidi yao zitachukuliwa.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa ni bora wananchi waache tabia hiyo ya
kujichukulia sheria mikononi kwani vyombo husika kama Polisi na Mahakama
vipo kwa ajili ya shughuli hiyo.