Mbunge Ally Kessy Achukizwa na Kitendo cha Roma Kumtukana Rais.
Mbunge
wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy amedai kuwa msanii Roma Mkatoliki
amerekodi wimbo ambao una lugha ya matusi dhidi ya Rais, na kulaani
kitendo hicho.
Akizungumza
leo bungeni mjini Dodoma, Kessy ambaye alionesha kuumizwa na kitendo
cha kuandika na kurekodi nyimbo zenye lugha za kuudhi dhidi ya Mkuu wa
nchi alihoji uhuru na demokrasia inayotoa nafasi hiyo.
“Wewe
unamtukana Rais wa nchi umekuwa nani? Uhuru gani, demokrasia gani hii.
Unaimba wimbo na mtu wa studio anarekodi, ama kweli huu sio utawala…
wangeniachia mimi dakika mbili niwaoneshe hawa,” amesikika Kessy.
“Haiwezekani,
Mkuu wa nchi anatukanwa. Ukiusikia huo wimbo wa Roma sijui Mkatoliki
ndugu zangu ni wimbo wa aibu. Haiwezekani mtu anaachia wimbo kama ule
halafu unamshabikia tu,” aliongeza.