HIVI NDIVYO WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ALIVYOWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS MHE.DKT. MAGUFULI.


Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara
baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Terminal One jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni
wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal
One jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili
Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.


Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa
mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar
es Salaam.

Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua
gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn
mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wanahabari mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini
Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza
na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini
Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.

Shamra shamra
zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam
Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal
2 jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto
Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam. PICHA NA
IKULU.


