Msanii Harmorapa amekiri kuwa
mtayarishaji mkongwe wa muziki Bongo P Funk Majani ndiye amembadilisha
kutoka kwenye uimbaji wa rap wa kizamani hadi kufikia kurekodi kiboko ya
mabishoo ambayo inaendana sawa na soko la muziki wa sasa.
Akiwa
Kikaangoni Harmorapa amesema kuwa baada ya kutoa ngoma ya kwanza
'Usigawe pasi' Majani alimtafuta na kumpongeza kuwa anajua kuandika
lakini bado uimbaji ni wa kizamani hivyo akaanza kumtengeneza ili kukaa
sawa.
"Unajua Majani ni legend
producer hapa nchini. mimi alinitafuta nilipoachia tu ngoma ya kwanza
usigawe pasi akaniuliza vipi, nikasema nina ngoma zingine nilizowahi
kurekodi nikamsikilizisha. Alinipongeza kwenye uandishi kwamba najua
kuandika ila tatizo lipo kwenye rap yangu kuwa ilikuwa ya kizamani sana
na kwamba muziki ni biashara, akaniambia kilichobaki kwangu ni training
tu ili nifanye poa"- Harmorapa.
Amesema baada ya ushauri na maelekezo
kutoka kwa Majani, nipo aliporekodi Kiboko ya Mabishoo, pamoja na ngoma
nyingine ambazo amesema zinatoka muda si mrefu, akiwa amebadilika
kabisa.
Harmorapa Afunguka Kuhusu Rap Yake....Akiri kuwa Majani Amembadilisha sana Kimuziki
Reviewed by Unknown
on
1:42 PM
Rating: 5