Baada ya Kula Ujana Vyakutosha..Aunty Lulu Sasa Aanza Kuisaka Pepo...Ubuyu wote Uko hapa.
Baada ya maisha ya ujana yenye kila aina ya uchafu hatimaye msanii na
Mtangazaji Lulu Semagongo maarufu kama Aunty Lulu, amesema anajiandaa
kuimba nyimbo za Injili zitakazozungumzia maisha yake ili watu wengine
wajifunze.
Aunty Lulu alisema nyimbo zake zitabadilisha maisha ya watu wengi kwani
ujumbe utakaokuwemo ndani yake utazungumzia mambo mengi ambayo amepitia
katika maisha yake.
“Najiandaa kuimba nyimbo za Injili na wimbo wangu wa kwanza utaitwa
Unikumbuke Mungu, ambapo ndani yake nitaeleza mambo yote niliyopitia
kwenye maisha yangu ikiwemo kubadilisha wanaume tofauti, starehe za kila
aina, kuvuta sigara na mengine mengi na nimeamua kufanya hivi ili
kupitia historia ya maisha yangu vijana wengi wabadilike,” alisema.