Aliyeandika 'Komela' ya Dayna adai sifa cake
Kwenye
story tatu ya Planet Bongo ya East Africa Radio Foby amedai kuwa
wasanii wengi wamekuwa wakiwabania waandishi wa wimbo kwa kushindwa hata
kutamka majina ya watu wanaoandika nyimbo zao.
Amewataka wasanii kubadilika na kuwataja hadharani watu waliowaandikia nyimbo zao huku akimtole mfano Dayna.
"Mimi nimemuandikia Dayna Komela imefanya vizuri sana lakini hajawahi kusema kama mimi ndo nimefanya kazi hiyo" Amesema Foby.
Pia amesimulia jinsi uandishi wa kazi hiyo ulivyomtesa hadi usiku "Nakumbuka
kazi yake niliifanya mpaka saa saba usiku, wakanishusha Afrikasana yeye
na Billnass walikuwa wanaenda kwenye birthday party ya Nuh Mziwanda
nikiwa nimeshamalizia kazi yake."
Foby pia amemtaja msanii mwingine ambaye alimuandikia ngoma na kushindwa kurudisha sifa
"Pia Seline naye nimemuandikia naona hanitaji labda kwa sababu bado
wimbo mpya huko mbeleni kama ataweza kunipa credit itapendeza sana, Sawa
umenilipa lakini unaponitaja inanipa faraja zaidi. Uandishi ni biashara
unaponipa credit leo kesho unaniongezea wateja wengi" Amesema Foby


