Wakili maarufu nchini, Peter Kibatala
amejitolea kumtetea mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego
aliyekamatwa jana mkoani Morogoro kutokana na kuimba wimbo unaokosoa
Serikali iliyopo madarakani.
Nay wa Mitego jana amekamatwa mkoani
Morogoro na amesafirishwa hadi jijini Dar es Salaam na kufikishwa
Central kutokana kosa hilo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wakili
Kibatala ameandika kuwa “Nay wa Mitego amefikishwa Central Police
Station, Dar es Salaam yuko salama na imara amekula pia. Kwa kuwa
amefika jioni sana; hakuna kinachoweza kufanyika leo Wakili Faraji
Mangula alifika pale, na kesho tutapigana afikishwe Mahakamani au apewe
dhamana.
WAKILI KIBATALA AJITOSA KUMTETEA MSANII NAY WA MITEGO.
Reviewed by Unknown
on
9:54 AM
Rating: 5