Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema,
watoto takriban milioni 1.4 nchini Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na
Yemen wako katika hatari ya kukabiliwa na njaa, na kuitaka jumuiya ya
kimataifa ichangie dola za kimarekani milioni 255 ili kutatua hali hiyo.
UNICEF pia imetahadharisha kuwa hatari ya njaa si kama tu iko katika nchi hizo nne.
Shirika hilo limesema kutokana na vurugu, njaa na ukosefu wa
maji, watu wanalazimika kukimbia makazi na kukimbia nchi, na kiwango cha
utapiamlo pia kitaendelea kuongezeka katika nchi jirani.
UNICEF pia imesema watoto waliokimbia makazi hawana huduma za afya na lishe, maji safi, au mazingira safi.
UNICEF:DOLA MILLIONI 255 ZAHITAJIKA KUWASAIDIA WATOTO WANAOKABILIWA NA NJAA AFRIKA.
Reviewed by Unknown
on
8:51 AM
Rating: 5