Umoja wa Mataifa (UN) umelaani vikali mauaji ya wafanyakazi sita wa kutoa misaada nchini Sudan Kusini.
Miongoni mwa waliouawa
ni raia watatu kutoka Kenya, na watatu kutoka Sudan Kusini ambao
walitekwa siku ya Jumamosi walipokuwa wakisafiri kutoka mji mkuu Juba
kwenda mji wa Pibor.
Hili ni tukio la tatu
la aina hiyo ndani ya mwezi mmoja likiwa limepoteza maisha ya watu wengi
tokea kuanza kwa mgogoro huo mwaka 2013.
Mkuu wa mashirika ya kibinaadam nchini Sudan Kusini Eugene Owusu ameelezea mauaji hayo kama uhalifu wa kutisha.
Wafanyakazi 12 wa
mashirika ya kutoa misaada waneuawa mwaka huu, wakati huu ambapo
wanajaribu kuelekea sehemu ambazo umaskini ni mkubwa kutokana na vita.
UN Yalaani Mauaji ya Watoa Misaada Nchini Sudan Kusini.
Reviewed by Unknown
on
10:12 AM
Rating: 5