Mkali wa Hip Hop Bongo, Billnass amesema
kuwa hakwenda kituo cha polisi kuwaangalia mabosi zake waliokuwa
wametuhumiwa kujishughulisha na madawa ya kulevya ili wajifunze maisha.
Billnass anayetamba na ngoma yake
‘Mazoea’ amesema katika maisha aliyoishi yeye suala la kwenda ndani ni
jambo la kawaida sana hivyo kutokwenda kuwaona maboss zake ambao ni Pet
Man na Mchafu Chakoma kipindi wamepatwa na matatizo si jambo la msingi.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa hawezi kuhama label yake ya (LFLG) kwa ajili ya maboss zake wamehusishwa na dawa za kulevya.
Kwa upande mwingine Billnass ameongeza
kuwa Mwana FA kumfunika katika wimbo wake wa Mazoea aliomshirikisha ni
heshima sana kwake kwa kuwa msanii huyo ni mkongwe kwenye muziki.
Pia msanii huyo amekanusha kuwahi kuwa na
mahusiano na msanii Linnah Sanga ambaye ukaribu wao ulifanya watu wengi
kuhisi kwamba ni wapenzi.
Sikiliza Alichoongea Billnass kuhusu Petit Man na Mchafu Chakoma
Reviewed by Mipiko
on
8:11 AM
Rating: 5