KIDEBE YA DOGO JANJA YAZIDI KUPIGA HATUA....YAJIWEKEA REKODI HII MPYA YOUTUBE
Miongoni
mwa vipimo vya video ya muziki kupokelewa vizuri ni pamoja na namba za
watu waliotazama au kupakua mtandaoni. Kwa kutumia kigezo hicho video ya
‘kidebe’ imepenya.
Video ya wimbo wa Dogo Janja ‘Kidebe’ imefanikiwa
kufikisha views milioni moja kwenye mtandao wa Youtube. Speed hii
inaweza kuifikisha mbali zaidi video hii ambayo ilianza kuonesha
mafanikio makubwa mara baada ya kuachiwa na kuifanya kuwa video ya Dogo
Janja iliyotazamwa zaidi kati ya video zake zote.
Kupitia mtandao wa Instagram, Dogo Janja ameandika, “The best is still yet to come.. #1MillionViews
Mpaka sasa ni miezi 5 imepita tangu video hiyo ilipowekwa kwenye mtandao huo mwezi 8 mwaka jana na imefanikiwa kutazamwa mara 1,000,735.


