Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewataka wadau wa mpira wa miguu nchini wapuuze taarifa za kwenye mitandao kuhusu mchezaji Venance Ludovick.
Suala la mchezaji huyo linaendelea kufanyiwa kazi na Kamati ya
Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji. Tunawahakikishia umma wa wapenda
soka nchini kuwa haki itatendeka kwa mujibu wa kanuni zinazoendesha
mashindano husika.
Mchezaji huyo analalamikiwa na timu ya Yanga kwa kucheza katika mechi
yao dhidi ya African Lyon iliyochezwa Desemba 23, mwaka huu katika
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara kufungana bao 1-1, huku kwa Lyon bao lao likifungwa na
mchezaji huyo.
Hata hivyo, mara baada ya mechi hiyo, timu ya Yanga ilikata rufaa
katika Kamati hiyo ikitaka timu hiyo ipokwe ushindi kutokana na
kumchezesha mchezaji huyo, ikidai kuwa hakukamilisha taratibu za usajili
kutoka katika timu ya Mbao FC ya Mwanza na kwamba bado alikuwa na
mkataba wa kuichezea timu hiyo.
TFF watoa taarifa kuhusu mchezaji Venance Ludovick
Reviewed by Mipiko
on
12:05 AM
Rating: 5