Miaka minne iliyoipita, viwavi waliteketeza mazao nchini Zambia.
Rais wa
Zambia Edgar Lungu, ametoa wito kwa kikosi cha jeshi la anga kusaidia
kukabiliana na uvamizi wa viwavi nchini humo. Zambia ilishuhudia tukio
kama hilo miaka minne iliyopita.
Wadudu
hawa wanateketeza mazao katika mikoa sita kati ya kumi inayounda nchi ya
Zambia. Wadudu hao wana uwezo wa kuharibu mashamba yote.
Ndege za kijeshi zimeanza zoezi la kupulizia dawa za kuua wadudu katika maeneo yaliyoathirika zaidi.
Miaka minne iliyoipita, viwavi waliteketeza mazao nchini Zambia, hasa mahindi, mihogo, mtama na mchele.