Raia wa Colombia wakishangazwa na matokeo ya kura ya maoni
Wapiga kura nchini
Colombia wamepinga katika kura ya maoni makubaliano ya kihistoria
yaliyofikiwa baina ya serikali ya nchi hiyo na kundi la waasi la FARC.
Zaidi ya watu milioni kumi na tatu wamepiga kura, lakini wanaopinga makubaliano hayo wameshinda kwa kura zisizozidi elfu sitini.
Rais
Juan Manuel Santos ambae ametia saini makubaliano hayo wiki iliyopita
katika sherehe zilizofana na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo
kiongozi wa FARC, amesema hatojiuzulu.
Ameongeza kusema, makubaliano hayo ya amani ambayo
yatamaliza mgogoro wa miongo mitano bado yanafanya kazi na kwamba yeye
atasimamia amani hadi siku yake ya mwisho ofisini.
Kwa upande
wake, kiongozi wa kundi la waasi FARC leader, Timochenko, amesikitishwa
na matokeo hayo na kusisitiza kwamba yeye pia anataka amani.
Wananchi Colombia wapinga makubaliano ya amani
Reviewed by Mipiko
on
5:33 PM
Rating: 5