WALICHOKIFANYA NAVY KENZO NA ALIKIBA..SOMA HAPA
Baada
ya KAMATIA CHINI pamoja na nyimbo ya GAME kupenya katika mipaka ya
Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kundi matata la muziki kutoka
TANZANIA linaloundwa na couples wawili AIKA pamoja na producer bora wa
mwaka 2015-2016 NAHREEL wameingia jikoni na kupika hits nyingine kibao
ikiwemo colabo ambayo tayari imefanywa pamoja na ali kiba
Miezi kadhaa nyuma Navy kenzo walitoa mipango yao ya kufanya colabo na
wasanii kutoka nje ya mipaka ya TANZANIA akiwemo PATORAKING na wengine
kibao
“Mmmh tuna nyimbo nyingi ukiacha hii na Ali kiba na tayari tuna nyimbo
ambayo tumesha shoot South Africa kwa Justin compus na ipo tayari kabisa
vile vile tuna colabo kibao kutoka nje ya mipaka ya TANZANIA ikiwemo
NIGERIA pamoja na South Afrika hivyo nadhani ni muda wa mashabiki wetu
kusubiri coz tumeandaa vitu vizuri kwa ajili ya kufunga nao mwaka.”
alisema AIKA
Lakini
pia Navy kenzo limekuwa kundi pekee ambalo limechaguliwa kutoka
TANZANIA kupeperusha bendera kwenye msimu mpya wa nne wa COKESTUDIO
AFRIKA ambayo inafanyikia nchini Kenya


