Breaking News

UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE UTAFANIKIWA KAMA HAYA YAKIZINGATIWA


UNGA LISHE :  Ni  unga bora na unao

hitajika sana  katika kuborehs afya  za

watoto, wazee na wagonjwa. Ukiwa  kama

mjasiriamali mdogo, ni muhimu kujua

namna  ya kutengeneza unga  lishe, kwani

malighafi zinazo tumika  katika

utayarishaji  wa unga huu zinapatikana

kwa wingi na kwa bei nafuu, hivyo basi

hata kwa wewe mwenye mtaji  mdogo,

unaweza kufanya  biashara hii bila ya

kuhitajika kuwa na mtaji mkubwa jambo

linalo chukuliwa  kama  changamoto  kwa

wajasiriamali

wengi nchini.

MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA KATIKA

UTENGENEZAJI  WA UNGA  LISHE.

* Karanga - Nusu Kilo.

* Soya - Nusu Kilo.

* Ulezi - Kilo moja na Nusu.

* Mahindi -Nusu Kilo

*Mtama - Mtama Nusu Kilo.

* Uwele - Nusu kilo.

* Mchele -  Nusu kilo..

JINSI YA KUTENGENEZA UNGA LISHE .

1. Safisha  ulezi na kuutoa michanga

pamoja na vumbi.

2. Kaanga  soya kwenye moto mpaka

ibadilike rangi na kuwa " brown " ama

kahawia.

3. Kaanga  karanga zako na toa maganda.

Saga  mchanganyiko wa malighafi zote

hapo  juu kwa pamoja, kisha anika juani

mpaka  ukauke, halafu weka kwenye

vifungashio kwa  ajili  ya kuuza.

MASOMO YA  KESHO  : Utengenezaji wa

Chilli  Souce, Tomato Souce, Mango

Pickles, Keki, Soya Masalla, Wine Ya

Ndizi, Wine Ya  Nanasi, Wine Ya Rossela,

Crips  za  Ndizi, Siagi Ya Karanga "

Peanut  Butter ', Chaki, Kiwi & Mkaa Kwa

Kutumia Makaratasi na  Vifuu  vya Nazi.

ENDELEA KUTEMBELEA BLOGU HII, MARA

KWA MARA KWANI  TUTAKUWA

TUKICHAPISHA  MASOMO YA

UTENGENEZAJI  WA BIDHAA ZOTE AMBAZO

TUMEZITANGAZA  KATIKA MATANGAZO

YETU  YA AWALI PAMOJA NA NYINGINE

ZA NYONGEZA  AMBAZO  HATUJA

ZITANGAZA.. KAMA  UNA SWALI  LOLOTE

LILE, MAONI, USHAURI AMA  UNA BIDHAA YOYOTE  AMBAYO  UNGEPENDA TUIWEKE HAPA BLOGUNI TAFADHALI WASILIANA NASI KUPITIA MTANDAO WA WHATSAPP @0768548165