Baada ya Rais John Pombe Magufuli kuzindua ndege mbili mpya
zitakazotumiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) mwezi uliopita,
shirika hilo limetangaza rasmi maeneo ya safari za ndege hizo ikiwa ni
pamoja na nauli.
Kupitia ukurasa wa Twitter wa shirika hilo waliandika kuwa nauli ya
safari ya ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ni shilingi laki moja
na sitini (160,000) ambapo nauli ya kutoka Dar es Salaam hadi Arusha ni
bei hiyo hiyo, laki moja na sitini (160,000).
Aidha, shirika limetahadharisha kuwa nauli hizo ni za kwenda tu, na
si kwenda na kurudi. Pia wameeleza kuwa nauli za safari kwenye mikoa
mingine bado hazijapangwa ila ndio wapo kwenye mchakato
SHIRIKA LA NDEGE LA AIR TANZANIA LATANGAZA NAULI ZAKE NI SAWA NA BURE
Reviewed by Mipiko
on
6:15 PM
Rating: 5