Rais Barack Obama
wa Marekani ameyaelezea malalamiko yaliyotolewa na mgombea kupitia chama
cha Republican, Donald Trump, kwamba kuna udanganyifu unafanyika katika
uchaguzi wa Rais nchini humo, kuwa ni ya hatari na kuharibu demokrasia.
Amemlaumu
mgombea huyo wa Republican kutilia shaka uhalali wa uchaguzi huo, bila
ya kuwa na ushahidi kamili wa kuwepo kwa hila kwenye uchaguzi huo
unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Wakati wa mdahalo wao wa
tatu na wa mwisho uliofanyika jana katika yake na mpinzani wake Hillary
Clinton, Bwana Trump alikataa moja kwa moja kusema kwamba atakubali
matokeo iwapo atashindwa.
Hata hivyo chama chake cha Republican kimekuwa kikijaribu kusafisha kauli yake hiyo.
Timu
ya Kampeni ya uchaguzi ya Bwana Trump inamlaumu Hillary Clinton mgombea
kupitia chama cha Democrats kwa kupanga jaribio la kutaka kumchafua
mgombea huyo wa Republican baada ya mwanamke wa 10 kujitokeza akiilaumu
tabia yake ya kudhalilisha wanawake kijinsia.
Mwana mama huyo
Karena Virginia anamtuhumu Bwana Trump kwa kile alichosema alimpapasa
kifuani, wakati wa mashindano ya mchezo wa tenisi mwaka 1998.
Obama asikitishwa na malalamiko ya Trump
Reviewed by Mipiko
on
5:25 PM
Rating: 5