Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ziara katika Hospitali za Wilaya ya Iramba Mkoani Singida
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya Iramba Mkoani
Singida na kukagua huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya pamoja na
Zahanati ya Kisimba ndani ya Wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.
Akiwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza kujionea huduma
mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza uongozi wa
Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa
malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.
“Mfumo
wa malipo ya kielektroniki umeleta ukombozi mkubwa sana kwenye
mahospitali nchini. Mapato yameongezeka. Udhibiti wa mapato umekuwa
rahisi. Nawaagiza nanyi Hospitali ya Iramba kuhakikisha munafunga mfumo
huu wa malipo wa kisasa hususani kwenye: Maabara,Chumba cha upasuaji
(Theatre), Dirisha la dawa, na sehemu zote zenye kuingiza mapato”.
Ameeleza Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.
Katika
Zahanati ya Kisimba ambayo ipo umbali wa zaidi ya Kilometa 10,
Dk.Kigwangalla ameweza kujionea huduma mbalimbali kwenye Zahanati hiyo
ambayo ni mpya huku ikiwa msaada mkubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo.
Picha chini ni Majengo ya Zahanati mpya ya Kisimba iliyopo Wilayani Iramba.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akisalimia wenyeji (Hawapo pichani) wakati
alipotembelea Zahanati hiyo ya Kisimba


