MAUA SAMA AYASEMA HAYA KUHUSU MUZIKI WAKE
Muimbaji wa Mahaba Niue,
Maua Sama amedai kuwa anaweza kufanya kazi na label yoyote ile
inayofanya vizuri na yenye mafanikio yanayoonekana.
Hata hivyo ameongeza
kuwa kwa sasa yupo chini ya usimamizi wa THT na kwamba si rahisi kuhama,
bali inawezekana kushirikiana na msanii yeyote nje ya uongozi wake.
Akiongea na kituo kimoja
cha redio nchini, Maua amesema so far THT imemfikisha sehemu nzuri na
haoni mapungufu yoyote kwenye muziki wake.
Kwa upande mwingine Maua amedai kuwa mashabiki wake watarajie kazi nzuri na mpya kutoka kwake.


