MAKONDA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA BUGURUNI JIJINI DAR LEO

Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa
hadhara uliofanyika leo jioni katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ili
kuzungumzia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Katika Mkutano huo Makonda amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele
katika kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza au kuondoa kabisa
changamoto zinazowakabili ikiwemo, vibaka, dadapoa na uchafu wa
mazingira, akisema, ikiwa wananchi watashitiki kikamilifu ni rahisi
kukomesha tatizo la vibaka kwa sababu vibaka na dadapoa wanatoka
miongoni mwa familia zao na hali kadhalika uchafu wa mazingira unatokana
na takataka wanazozalisha wananchi wenyewe.

Kamanda
wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero
na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uliofayika leo jioni Buguruni kwa
Mnyamani

Viongozi
waandamizi katika Wilaya ya Ilala, wakimsikiliza mkuu wa mkoa Paul
Makonda wakati akihutubia wananchi katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani
leo jioni. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela
Palela, Ofisa Tawala wa Manispaa hiyo, Edward Mpogolo, Naibu Meya
Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Segerea wilayani humo Bona
Kalua

Mjumbe
wa Shina namba tano, Katika Kata ya Myamani, Buguruni Zubeda Lugiga,
akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara
leo jioni

Mkazi
wa Buguruni, Sadik Mgaya akieleza changamoto na kero zinazowakabili
wananchi wa eneo hilo wakati wa mkutano huo wa Makonda.


