JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI
Hujambo mpenzi msomaji na karibu sana katika ukurasa huu ambao pamoja na
habari tutakuwa tunajifunza mambo mbalimbali ambayo yanaweza kutusaidia
kujikwamua na umaskini.Kama mna kumbukumbu nzuri,siku za karibuni
nimekuwa nikiwaambia kuwa nitawaletea masomo ya jinsi ya kutengeneza
bidhaa mbalimbali za viwandani.Leo katika somo letu tutaanza kujifunza
jinsi ya kutengeneza BATIKI na naomba mnifuatilie kuanzia mwanzo mpaka
mwisho wa masomo haya na myafanye kwa vitendo na MUNGU atawabariki.
MAHITAJI:
1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.
2.Sponji zenye urembo mbalimbali.
3.Brash kubwa/ndogo.
4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.
5.Sufuria.
6.Vitambaa vya mpira.
7.Misumari midogo.
8.Jiko.
MADAWA:
1.Sodium hydrosulphate.
2.Caustic soda
3.Mshumaa.
KAZI ZAKE:
1.Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa
na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana
moja nyingine haifanyi kazi.
2.Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa
kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina
yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.
JINSI YA KUTENGENEZA.
(a)JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:
Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoekidogo.Andaa kitambaa
cha cotton na kukitandika mezani,chovya kibao chenye picha kwenye
mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo.Endelea
kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.
(b)JINSI YA KUWEKA RANGI:
Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka
sita.Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate
vijiko vinne mpaka vitano.Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko
kimoja.Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na
mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu.Tumbukiza vitambaa vya
vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa
dakika kumi mpaka kumi na tano.Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye
kivuri ili mshumaa usiyeyuke.
(c)KUWEKA RANGI YA PILI:
Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi
tu.Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani
uleule,
Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima
rangi kwa kufuata hatua zilezile.Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa
mda uleule kisha anika.
(d)JINSI YA KUFUA MSHUMAA:
Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga
jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza
kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.
PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.


