Mkali wa wimbo ‘Salome’ na Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz
amesema uwekezaji mkubwa alioufanya katika label yake ya ‘WCB’ hauwezi
kumlipa kwa muda mfupi.
Diamond akiwa na Rayvanny
Label hiyo ambayo kwa sasa inafanya vizuri katika muziki ina wasanii 4, Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny pamoja na Queen Darlin.
Akiongea katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Diamond alisema label hiyo kwa sasa inatumia pesa nyingi kuliko kuingiza.
“Bado sana haiwezi kulipa kwa muda mfupi, itachukua mwaka mmoja mpaka
miwili ndo inanze kulipa lakini sasa hivi bado,” alisema. “Lakini
furaha yangu ni kuona wasanii wa WCB wanaanza kuwa nominated kwenye tuzo
tofauti tofauti za Afrika, nyimbo zao zinatambulika katika nchi tofauti
za Afrika, wanatambulika na wasanii tofauti tofauti wa Afrika, so hicho
ndio kitu ambacho nilikuwa nakipigania,”
Pia muimbaji alisema ameamua kusaidia wasanii kwanza halafu suala la
mapato litakuja baadae wakati wasanii wapo kwenye ramani ya muziki.