BSS Kuna Uchawi Gani? Mbona Wengi Hawafanikiwi?

Tuchukulie mfano mtu kama Jumanne Idd mpaka leo hajulikani halipo alkadharika Walter Chilambo, Kayumba , AngelMarry Kato , Steven Lupenza, Nasibu Fonabo nk ni miongoni mwa vijana ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuimba lakini cha ajabu hawafanikiwi kulinganisha na washiriki wengine kama vile Harmonize ingawa alitoka mapema na kuonekana si chochote leo hii katudhihirishia kwamba yeye ana uwezo gani....
By Hance mtanashati
Jibu la Mdau
Kwanza ni jambo la kujiridhisha kuwa si BSS tuu bali hata huko nje shows
kama za the voice, SA idols, xfactors, na Got talents za nchi nyingi,
ni watu wachache sana walio shinda mashindano ya aina hii wame make ki
muzik.
Kwanini!!?
1. Lengo la mashindano, waandaji huwa wanaandaa kwa ajili ya faida yao
na kupata wadhamini, na mara nyingi wakisha maliza shindano hawawekezi
kwa nguvu kubwa kwani kuna shindano la mwakani inabidi waandae tena,
hawana time na wewe
Pia washindanaji lengo lao kubwa zaidi ni kupata yale mamilioni tuu, wakisha pewa kuna msemo unasema easy come easy go
2. Mashabiki wa mashindano, askudanganye mtu, watanzania wanao fuatilia
BSS ni chini ya milioni 10, wanao piga kura ni chini ya laki moja, kwa
hiyo kama msanii ukishinda unakuwa hujapata fan base kubwa bado isipo
kuwa ki portion kidooogoo cha wale walio angalia na wakajisumbua hata
kupiga kura,,na wengi wanai piga kura huwa wanaanza kwanza kukuonea
huruma ya kimaisha mfano unakumbuka Jumaanne Idd kwa hiyo Raymond akitoa
wimbo mmoja uka hit anapata fan base kubwa kuliko wewe mshindi
3. Mziki ni zaidi ya kukopi nyimbo za watu, angalia yule mshindi wa
mwaka jana kayumba alishnda kwa kuimba imba taarab za kina isha mashauz
sasa je akitoka BSS ana uweza huo mziki!!? Mpaka yeye mwenyewe hajui
afanyeje yaani
*Sababu ni nyingi lakini kikubwa ni wasanii wajiamini wahue uwezo wao ni
zaid ya kuimba BSS, ndio maana mara nyingi unakuta wanao fanikiwa ndio
wale walio shika u tano, au ukumi, kwa kuwa it takes more than to win
BSS ili kuwa msanii


