Breaking News

VIDEO:DIAMOND AFUNGUKA KUWA HATAKI TIFFAH AWE MSANII, ATALIWA SANA NA WANAUME



Diamond Platnumz amefunguka kwa kudai kuwa hataki mtoto wake wa kike Tiffah awe msanii kwa madai akiwa msanii atatembea kimapenzi na wanaume wengi.

Muimbaji huyo amedai mtoto wake huyo akiwa msanii, wanaume wengi watamiminika kumtaka kimapenzi.

“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana,” alisema Diamond weekend iliyopita  akiwa katika kipindi KTN nchini Kenya. 

“Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha,”

Aliongeza, “Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na kweli nimetulia,”

Muimbaji huyo leo Jumanne anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zari, Ivan aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa wa moyo.