PROF. JAY ALIA NA SHERIA YA HATI MILIKI...ADAI WASANII WENGI WA BONGO WAMEKATA TAMAA.
Prof.
Jay amebainisha hayo muda mchache alipotoka katika kikao cha Bunge na
kusema serikali inapaswa kuzingatia kilio hicho cha wasanii kwa
kusimamia kuwepo kwa hati miliki ili kuweza kuongeza pato la taifa
kupitia kazi za wasanii.
“Kilio kikubwa cha wasanii
wa Tanzania sasa hivi ni kuhusu masuala yao ya hati miliki na ukiangalia
Sheria ya hati miliki namba 7 ya mwaka 1999 imeonekana kuwa na
mapungufu makubwa sana, kiasi kwamba wasanii watanzania hawapati kile
kinachostahili, hawapati jasho lao linavyotakiwa na wasanii wa Tanzania
wamekata tama lakini kiukweli kabisa takwimu na tafiti zilizofanywa na
‘Lulu Art Promoters’ inaonyesha kwamba wasanii wa Tanzania na sanaa ya
muziki pekee yake inachangia zaidi ya asilimia 1 ya pato la taifa”. Alisema Mbunge huyo
Aidha, Prof. Jay aliendelea kwa kusisitiza kwamba “Muziki
ni nyanja muhimu sana, kiukweli ikitupiwa jicho na kuweza kupewa
kipaumbele wasanii wanaweza wakupata kile kinachostahili ili kuongeza
pato kubwa katika taifa letu.” Alisisitiza Prof. Jay


