Magari
matano ya Chama cha Wananchi (CUF) yanayodaiwa kufichwa na baadhi ya
wafuasi wa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sheriff Hamad miezi
kadhaa iliyopita yamepatikana maeneo ya Kimara-Bonyokwa jijini Dar es
Salaam.
Mmoja kati
ya walinzi wa CUF wa makao makuu ya ofisi za chama hicho, Jamal Yasin
amedai kuwa magari hayo yamepatikana katika nyumba ya mfuasi wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye hakumtaja jina na kwamba
yanasafirishwa na kuletwa kwenye makao makuu ya ofisi za CUF yaliyopo
Buguruni.
Yasin ameuambia mtandao huu kuwa, “Mchanjama
alitoa taarifa ya sehemu iliyokuwepo magari kwamba ni maeneo ya
Bonyokwa katika nyumba ya mfuasi wa Chadema jina lake halijajulikana,
kundi la wanachama wanayarudisha ofisini Buguruni.”
Ametaja baadhi ya magari hayo kuwa ni Landcruiser na Toyota.
Wafuasi wa Prof. Lipumba wakamata magari ya CUF yaliyofichwa
Reviewed by Mipiko
on
6:12 AM
Rating: 5